Kuhusu Translink

Tunaratibu na kuwasilisha huduma za basi, gari la moshi, mashua pamoja na huduma za tramu katika maeneo yote Kusini Mashariki mwa Queensland ikiwemo ni pamoja na huduma za basi katika Cairns katika Kaskazini mwa Tropical Queensland.

Pia tunalojukumu la kutoa maelezo kwa wateja, tikiti na mijengo ya huduma ya usafiri wa mali ya umma.

Eneo la huduma zetu

Kusini Mashariki mwa Queensland

TransLink hutoa huduma zake katika maeneo 23 pamoja na maeneo 7 katika Kusini Mashariki mwa Queensland. Mfumo wetu katika Kusini Mashariki mwa Queensland huenea kutoka eneo la Gympie iliyo kaskazini mwa Coolangatta katika kusini na magharibi mwa eneo la Helidon.

Cairns

Mfumo wetu katika eneo la Cairns hufahamika na Baraza la Eneo la Cairns. Hii imeenea kutoka eneo la Palm Cove kaskazini, kusini hadi eneo la Gordonvale na magharibi mwa eneo la Redlynch ikiwemo pamoja na Jiji la Cairns pamoja na maeneo yanayolizunguka Jiji la Cairns.

Eneo la huduma zetu.

Maelezo ya usafiri

TransLink inahusu kuunganisha watu na mahali.

Ikiwa wewe unatembelea Queensland au wewe ni mwenyeji, unayetembelea mazingira ya Kusini Mashariki mwa Queensland na Cairns ukitumia huduma za usafiri wa mali ya umma ni rahisi.

Huduma na ratiba

Utapata huduma za basi, gari la moshi, mashua na huduma za tramu pamoja na ratibaramani pamoja na maelezo ya mwisho wa safari, ikiwemo ni pamoja na kila kitu utakachohitaji ili kujua kuhusu Tikiti na nauli pamoja na jinsi ya kutumia basi, gari la moshi, mashua au tramu kwa kutumia ‘jinsi ya’ mwelekezo.

Pia tunayo maelezo zaidi kuhusu:

Mpango wa safari

Tumia mpango wa safari ili kupanga safari yako.

Weka nambari ya mtaa pamoja na jina la mtaa (kwa mfano, 16 Mtaa wa Smith) ikiwem ni pamoja na jina la mtaa katika nafasi ya mtaa. Pia unaweza kutafuta eneo la ardhi au jina la kituo cha basi, gari la moshi au kituo cha tramu au kituo cha mashua katika nafasi cha pili. kwa mfano, unaweza kutafuta The Gabba, Uwanja wa Ndege wa Brisbane, Kituo cha Soko ya Cairns Katikati au kituo cha Enoggera.

Kutembelea Queensland

Kutembelea Kusini Mashariki mwa Queensland

Unaweza kusafiri kwenye mfumo wa TransLink wa Kusini Mashariki mwa Queensland ukitumia seeQ cardGold Coast go explore cardgo card au tikiti ya karatasi ya usafiri wa mara moja.

go card haizidi bei gharama ya chini kuliko asilimia kuliko bei ya tikiti moja ya karatasi. Soma zaidi kuhusu nauli ya sasa hiviKonsesheni pamoja na bei nafuu pamoja na njia za kuweka akiba pesa.

seeQ card ni njia rahisi ya kusafiri na kugundua eneo la Kusini Mashariki mwa Queensland. Ukitumua seeQ card, wewe utapata tikiti ya siku 3 au 5 kwenye huduma ya Translink. Soma zaidi kuhusu seeQ card.

Gold Coast go explore card ni njema kwa wageni wanaotembelea Gold Coast. Hii hutoa usafiri wa siku moja mzima kwenye basi pamoja na tramu, ikiwemo pamoja na huduma za theme parks pamoja na Uwanja wa Ndege wa Gold Coast, kwenye Gold Coast pekee. Soma zaidi kuhusu Gold Coast go explore card.

Kutembelea Cairns

Safiri ukitumia Tikiti ya Karatasi ya Cairns ya kila siku au kila wiki au wiki . Tafadhali rejelea kwa tiikiti, nauli pamoja na maeneo katika Cairns kwa maelezo zaidi.

Tikiti na nauli

Tikiti, nauli na maeneo katika Kusini Masharikki mwa Queensland

Aina za Tikiti

Safiri kwenye huduma za TransLink katika Kusini Mashariki mwa Queensland ukitumia go card au ikiwa wewe ni mgeni, seeQ card or Gold Coast go explore card (kwa usafiri wa basi pamoja na tramu katika eneo la Gold Coast pekee). Pia unaweza kununua tikiti ya karatasi ya usafiri wa mara moja.

go card

go card ni tikiti ya umeme ambayo hukuitikisha wewe kusafiri kwenye kubadilisha aina ya usafiri kote katika TransLink katika huduma za usafiri wa basi, gari moshi, feri pamoja na huduma za tram katika Kusini Mashariki mwa Queensland.

Ni rahisi kutumia na itahesabu nauli inayofaa ikiwemo pamoja na ubadilishaji wa usafiri, usafiri wa ‘off-peak’ pamoja na bei nafuu kwa abiria safiri wanaosafiri mara kwa mara, wewe unaweza kustahili na kuitoa kutoka kwa mabaki yaliyoko kwenye kadi yako.

Ongeza pesa mara kwa mara katika kadi yako nearest go card iliyokukaribia au pangia auto ongeza pesa kwenye kadi ili uweze kupata pesa za usafiri.

Tafadhali rejelea kanuni na masharti ya go card kwa maelezo zaidi.

Jinsi ya kutumia go card

Unapoingia basi au feri, au unapoingia eneo la kituo cha gari moshi au tramu, gusisha kadi yako ya go card yako kwenye kidunde huku ikielekea juu ilikuigusisha. Rudia kwa kuigusisha kadi unapotoka.

Ikiwa unashuka na kuingia basi, gari la moshi, mashua ya kuvushia au huduma za tramu nyingine, hakikisha kuwa unagusisha kadi yako unaposhuka na ungusishe unapoingia kwenye huduma ya usafiri inayofuatia.

Angalia mataa na usikilize bipu:

 • Mtu mzima - mwangaza wa rangi kijani kibichi, bipu 1
 • Mtoto, mzee mstaafu, konsesheni – mwangaza wa rangi ya machungwa, bipu 2

Nauli iliyo sahihi hutolewa kutoka mabaki ya pesa katika kadi yako na mabaki yaliyobaki yataonyeshwa kwenye kioo cha mashine ya kusoma kadi wakati unapoigusisha kadi yako.

Tafadhali rejelea kwenyemwongozo kwa matumizi ya go card kwa maelezo zaidi.

Mahali pa kununua au kuongeza pesa kwenye kadi yako ya go card

Nunua go card:

 • tuvuti
 • katika duka lolote la 7-Eleven
 • ofisi ya kununua tikiti katika kituo cha gari la moshi
 • busway pamoja na mashine za nauli katika kituo cha tramu
 • wachuuzi walioteuliwa ikiwmo ni pamoja na duka za ajenti wa magazeti pamoja na duka za bidhaa za jumla

Tafuta eneo lililokaribia au pigia 13 12 30 wakati wowote, masaa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki.

Tikiti ya karatasi ya usafiri wa mara moja

Tikiti ya karatasi ya usafiri wa mara moja tu ni tikiti ya usafiri wa mara moja inayotumiwa na watumizi wa usafiri wa umma au wageni wa muda mfupi, na inatumika katika basi, gari la moshi, mashua pamoja na tramu katika Kusini Mashariki mwa Queensland. Unaweza kununua tikiti ya karatasi ya usafiri wa mara moja katika basi na mashua na kutkoa vituo vya gari la moshi na tramu.

Nauli

Ili kuhesabu nauli yako wakati unaposafiri katika Kusini Mashariki mwa Queensland, angalia maeneo unayopitia wakati wa safari yako. Toa eneo la chini utakalosafiria, ukianza kutoka eneo la juu zaidi, halafu uongeze moja. Virai hii ya hesabu huhesabu nambari sahihi za maeneo ambayo utayogharamika. Pia unaweza kutumia mpango wa safari to calculate the fare for a specific journey.

Maeneo

TransLink hutoa huduma zake katika maeneo 23 ya Kusini Mashariki mwa Queensland. Nauli ni mahesabu katika aidha kiwango cha mtu mzima au kiwango cha konsesheni na hutokana na idadi ya maeneo unayopitia wakati wa safari yako.

Mfumo wa maeneo hufanya kazi kwa mwelekezo mviringo, kuanzia eneo la 1 katika eneo la CBD la mji Brisbane pamoja na kuendelea hadi kaskazini mwa Sunshine Coast na Gympie, kusini mwa eneo la Gold Coast na kaskazini mwa Helidon.

Tafadhali rejelea kwenye nauli za sasa pamoja na nauli za maeneo kwa maelezo zaidi.

Tikiti, nauli pamoja na maeneo ya Cairns

Tikiti ya usafiri wa mara moja, kila siku au kila wiki zinapatikana kwa kununua kwenye basi katika eneo la Cairns

Nauli ni kutokana na idadi ya maeneo yaliyovukwa. Kunayo maeneo 11 katika Cairns. Eneo la CBD lipo katika eneo maalum (20) likiwa ni pamoja na maeneo 10 yanayoelekea hadi Palm Cove upande wa kaskazini, Gordonvale katika upande wa kusini pamoja na Redlynch iliyo magharibi.

Tafadhali rejelea ramani ya Mtandao wa eneo la Cairns na mahesabu ya nauli ya eneo na nauli ya sasa, to calculate the correct number of zones and ticket price ili kuhesabu idadi sahihi ya maeneo pamoja na bei ya tikiti.

Pia tunayo maelezo zaidi kuhusu

Jinsi ya kutumia basi

Kabla ya kusafiri

Kupanda kwenye basi

 • Simama katika kituo cha basi mahali ambapo dereva ataweza kukuona.
 • Inua mkono wako ili kujulisha dereva kuwa unataka kupanda basi (ita).
 • Kuwa na go card, seeQ card au Gold Coast go explore card (kwa usafiri wako kwa basi na tramu katika eneo la Gold Coast pekee), tikiti au pesa za nauli zilizo sahihi kabla ya kupanda.13]
 • Ikiwa wewe unasafiri kwa kutumia nauli ya konsesheni, hakikisha kuwa kadi yako ya konsesheni ipo nawe wakati wote.
 • Wakati unapoipanda, gusisha kadi yako ya go card, seeQ card au Gold Coast go explore card kwenye mashine ya kusoma kadi iliyo kwenye basi, onyesha tikiti yako uliyoinunua hapo awali kwa dereva wa basi, au nunua tikiti unapoipanda basi – jinsi ya kununua tikiti.
 • Wapishe abiria wanaoshuka basi.
 • Huduma zingine za basi huwa pre-paid na zitakuwa na herufi ya ‘P’ mbele ya nambari ya njia ya safari. Lazima uwe na go card, seeQ card au tikiti ya karatasi iliyonunuliwa hapo awali ili kupanda basi. Abiria walio na go card au seeQcard wanaweza kupanda kupitia milango ya mbele au nyuma. Abiria walio na tikiti ya karatasi lazima wapande kutoka sehemu ya mbele.

Kusafiri kwa basi

 • Baada ya kupanda, kwanza sogea ukielekea sehemu ya nyuma ya basi. Ikiwa hakuna viti vilivyo huru, shikilia kwenye vilivyofanywa usalama au kizuizi
 • Kila mara patia kiti chako kwa abiria walio na mahitaji maalum, kama vile watu walio na ulemavu, wazee, wanawake wenye mimba au wazazi wanaosafiri na watoto wachanga.
 • Ili kulishuka basi, bwenyeza kengele ya ‘kusimamisha’ kabla ya mita 100 kabla ya kituo unachoshuka. Ikiwa hauna uhakika kuhusu mahali unaposhuka, ulizqa dereva wakati unapoipanda basi.
 • Tumia milango ya nyuma unaposhuka basi, ikiwezekana.
 • Gusisha kadi yako ya go card, seeQ card au Gold Coast go explore card (kwa usafiri wako katika eneo la Gold Coast pekee) kwenye mashine ya kusoma kadi wakati unapokuwa unashuka kutoka kwa basi.
 • Ikiwa unashuka na kuingia basi, gari la moshi, mashua ya kuvushia au huduma za tramu nyingine, hakikisha kuwa unagusisha kadi yako unaposhuka na ungusishe unapoingia kwenye huduma ya usafiri inayofuatia.
 • Angalia TransLink kwa masharti ya usafiri.

Jinsi ya kutumia gari la moshi

Kabla ya kusafiri

Kupanda gari la moshi

 • Katika kituo cha gari la moshi, gusisha kadi yako yago card au seeQ card kwenye mashine ya kusoma kadi iliyo karibu na geti au kwenye jukua la kituo, onyesha tikiti yako uliyoinunua hapo awali kwake wa mkuu wa kituo au afisa wa tikiti, au nunua tikiti jinsi ya kununua tikiti.
 • Ikiwa wewe unasafiri kwa kutumia nauli ya konsesheni, hakikisha kuwa kadi yako ya konsesheni ipo nawe wakati wote.
 • Wakati wote, gojea gari la moshi katika jukua, na ubaki nyuma ya laini ya rangi ya manjano.
 • Wapishe abiria wanashuka.

Kusafiri kwa gari la moshi

 • Baada ya kuingia, songea nyuma kupitia njia baina ya viti huku ukienda mbali na milango.
 • Ikiwa hakuna kiti kisichokeliwa, hold on to a fitted safety handle or barrier.
 • Kila mara kipatie kiti chako kwa abiria walio na mahitaji maalum, kama vile watu walio na ulemavu, wazee, wanawake wenye mimba au wazazi wanaosafiri na watoto wachanga.
 • Gusisha kadi yako ya go card, au seeQ card kkwenye mashine ya kusoma kadi wakati unapokuwa unatoka nje ya kituo cha gari la moshi.
 • Ikiwa unashuka na kuingia basi, gari la moshi, mashua ya kuvushia au huduma za tramu nyingine, hakikisha kuwa unagusisha kadi yako unaposhuka na ungusishe unapoingia kwenye huduma ya usafiri inayofuatia.
 • Angalia TransLink kwa masharti ya usafiri.

Jinsi ya kutumia mashua

Kabla ya kusafiri

Kupanda mashua

 • Katika kituo maalum cha mashua, ungana au unda mlolongo kando ya njia ya kutembea na ukae upande wa kushoto ili abiria wanaoshuka waweze kupita upande wa kulia.
 • Wapishe abiria wanashuka.
 • Panda huduma hii wakati mataa makuu ya mashua yanapoonyesha kuwa ni salama kufanya hivyo.
 • Wakati unapoingia, gusisha kadi yako ya go card au seeQ card kwenye mashine ya kusoma kadi iliyo kwenye mashua, onyesha tikiti yako uliyoinunua hapo awali kwa muuzaji wa tikiti, au nunua tikiti unapoipanda mashua – jinsi ya kununua tikiti.
 • Ikiwa wewe unasafiri kwa kutumia nauli ya konsesheni, hakikisha kuwa kadi yako ya konsesheni ipo nawe wakati wote.

Usafiri katika mashua

 • Baada ya kuingia, tafuta kiti ndani au ndani katika eneo lililoteuliwa kuwa nje.
 • Ikiwa hakuna viti zinazopatikana, shikilia kwenye mpini uliwekwa kwa sababu ya usalama, au kizuizi.
 • Kila mara kipatie kiti chako kwa abiria walio na mahitaji maalum, kama vile watu walio na ulemavu, wazee, wanawake wenye mimba au wazazi wanaosafiri na watoto wachanga.
 • Kulingana na mwisho wa safari yako, wewe unaweza kuhitajika kushuka kupitia mlango wa mbele au mlango wa nyuma wa mashua ya kuvushia - tangazo litatangazwa ili kukujulisha wewe.
 • Gusisha kadi yako ya go card au seeQ card kwenye mashine inayosoma kadi unapokuwa unatoka kwenye mashua.
 • Ikiwa unashuka na kuingia basi, gari la moshi, mashua ya kuvushia au huduma za tramu nyingine, hakikisha kuwa unagusisha kadi yako unaposhuka na ungusishe unapoingia kwenye huduma ya usafiri inayofuatia.
 • Angalia TransLink kwa masharti ya usafiri.

Jinsi ya kutumia tramu

Kabla ya kusafiri

Kupanda tramu

 • Katika kituo cha tramu, gusisha kadi yako ya, go card, seeQ card au Gold Coast go explore card (kwa usafiri kwa basi au tramu katika eneo la Gold Coast pekee) kwenye mashine ya kusma tikiti katika jukua la kituo au nunua tikiti ya karatasi ya usafiri - jinsi ya kununua tikiti.
 • Ikiwa wewe unasafiri kwa kutumia nauli ya konsesheni, hakikisha kuwa kadi yako ya konsesheni ipo nawe wakati wote.
 • Subiri tramu katika jukua na ubaki umesimama nyuma ya laini ya rangi ya manjano wakati wote.
 • Wapishe abiria wanashuka.

Kusafiri katiika tramu

 • Baada ya kuingia, songea nyuma kupitia njia baina ya viti huku ukienda mbali na milango.
 • Ikiwa hakuna viti zinazopatikana, shikilia kwenye mpini uliwekwa kwa sababu ya usalama, kizuizi au keti chini.
 • Kila mara kipatie kiti chako kwa abiria walio na mahitaji maalum, kama vile watu walio na ulemavu, wazee, wanawake wenye mimba au wazazi wanaosafiri na watoto wachanga.
 • Gusisha kadi yako ya go card, seeQ card au Gold Coast go explore card (kwa usafiri wako katika eneo la Gold Coast pekee) kwenye mashine ya kusoma kadi wakati unapotoka nje ya kituo cha tramu.
 • Ikiwa unashuka na kuingia basi, gari la moshi, mashua ya kuvushia au huduma za tramu nyingine, hakikisha kuwa unagusisha kadi yako unaposhuka na ungusishe unapoingia kwenye huduma ya usafiri inayofuatia.
 • Angalia TransLink kwa masharti ya usafiri.

Utumizi wa shubaka ya kuwekea kibao cha kuchezea katika mawimbi

 • Kikomo cha urefu wa vibao vya kuchezea katika mawimbi katika usafiri wa tramu ni futi 6..
 • Shubaka ya kuwekea kibao chako cha kuchezea katika mawimbi huwa kimekaribia behewa za katikati za tramu. Behewa hizi hujulikana kwa kibandiko kilichokaribia mlango.
 • Tafadhali jaribu kuingia kwenye tramu karibu iwezekanavyo na behewa hizi za tramu, ili kuhakikisha kuwa umekiweka kibao chako cha kuchezea katika mawimbi haraka iwezekanavyo.
 • Weka kibao chako cha kuchezea katika mawimbi kwa uangalifu kwenye shubaka ya kuwekea mizigo hadi uwasili kwenye mwisho wa safari yako.

Wasiliana nasi na usaidie

TransLink inahusu kupatanisha watu na mahali. Kwa usaidizi zaidi, ili kuuliza swali au ili kupata majibu, tafadhali soma maelezo yaliyo hapa chini:

Tuvuti

Uliza maswali na utupe majibu yako kupitia fomu zetu zilizo kwenye tuvuti.

Angalia huduma za kisasa kwa ajili ya kujua basi ya saa hizi na wakati ujao, gari la moshi, mashua ya kuvushia pamoja na maelezo ya tramu.

Taarifa ya uwekaji wa siri 
Ikiwa inahusu go card yako, tupigie simu badala ya kuweka fomu. Tunahitaji kuongea na wewe kwa sababu ya mahitaji ya uwekaji siri.

Simu

 • Pigia simu 13 12 30 kutoka kwa simu ya nymbani mahali popote nchini Australia kwa gharama isiyobadilika ya kupiga simu zinazoanza na nambari 13. Gharama ya juu zaidi ya kupiga simu inaweza kuweko kwa simu zinazopigwa kwa kutumia simu ya mkono.
 • Kwa wapiga simu kutoka nchi za ng’ambo - pigia simu +61 7 3851 8700.
 • Wapiga simu Wasio-Ongea Kiingereza: Pigia simu 13 12 30 na uombe mkalimani ahusike na mazungumzo yako.
 • Huduma ya Kimataifa ya Relei (National Relay Service) (ikiwa wewe ni kiziwi au unayo hali ya kusikia/kuongea iliyodhoofika) TTY: Pigia simu 13 36 77 na ulizia 13 12 30.
 • Ongea na Sikiliza (relei ya maongezi-kwa-maongezi relay): Pigia simu 1300 555 727 na ulizia 13 12 30.
 • Relei ya Tuvuti: ungana na Huduma ya Kimataifa ya Relei (National Relay Service) na ulizia 13 12 30.

Hata kama tunakuuliza uwasiliane nasi moja kwa moja kwa mahitaji yako yote ya usafiri wa mali ya umma, kunaweza kuwa na wakati ambao utahitaji kuwasiliana moja kwa moja na opereta, ikiwemo ni pamoja na kutafuta mali iliopotea, usafiri wa shule na maulizo ya ufikikaji.